Bunge la Umoja wa Afrika
Bunge la Umoja wa Afrika ni mkutano wa wawakilishi wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika.
![](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/sw/thumb/7/78/Panafricanparliament.jpg/300px-Panafricanparliament.jpg)
Wabunge wake 265 hawapigwi kura na raia wa nchi wanachama bali wanateuliwa na bunge za nchi wanachama. Kwa sasa kazi ya bunge ni kutoa ushauri tu kwani haina mamlaka ya kutunga sheria.
Makao makuu ya bunge yapo mjini Midrand (Afrika Kusini, sasa kwa muda katika jengo la Gallagher Estate katikati ya Johannesburg na Pretoria. Afrika Kusini inalipa gharama za makao na za ofisi ya bunge.
Mkutano wa kwanza ulifanyika Machi 2004. Mwenyekiti wa kwanza wa bunge hilo alikuwa Gertrude Mongella kutoka Tanzania.
Ana makamu wanne kutoka kanda nne za Afrika, nao ndio:
- F. Jose Dias Van-Du’Nem kutoka Angola (Afrika ya Kusini)
- Mohammed Lutfi Farhat kutoka Libya (Afrika ya Kaskazini)
- Loum N. Neloumsei Elise kutoka Chad (Afrika ya Kati)
- Theophile Nata kutoka Benin (Afrika ya Magharibi)
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |
🔥 Top keywords: Maalum:TafutaMwanzoClatous ChamaUfahamu wa uwezo wa kushika mimbaShairiAina za manenoVivumishiJumuiya ya Afrika MasharikiKamusiFasihi simuliziNahauOrodha ya makabila ya TanzaniaKisaweSentensiMikoa ya TanzaniaMshororoKamusi za KiswahiliNembo ya TanzaniaTanzaniaOrodha ya mikoa ya Tanzania kwa eneoDiamond PlatnumzNominoMisemoAlama ya uakifishajiMadawa ya kulevyaKumaOrodha ya Mawaziri Wakuu wa TanzaniaSimba S.C.MofimuNgeliSilabiMfumo wa mmeng'enyo wa chakulaVitenzi vishirikishi vikamilifuKitenzi kishirikishiMaumivu ya kiunoHistoria ya TanzaniaVitendawiliKitenziUandishi wa ripoti