Rada
Rada (ing. radar) ni jina kwa mitambo inayotumia mawimbi ya redio kutambua vitu na vyombo mbalimbali kwa kuangalia mambo kama aina, mwelekeo, kasi n.k.
Rada hutumika kuchunguza ndege, meli, roketi, magari, mawingu katika utabiri wa hali ya hewa, n.k.
Mfumo wa rada unatumia transimita kuzalisha mawimbi ya umeme na sumaku aina ya redio na antena ya kurusha na antena ya kupokea (mara nyingi antena hiyohiyo hutumika kwa kurusha na kupokea) na chombo cha kupokea na kutafsiri kitu kinachochunguzwa.
Rada iliundwa na mataifa kadhaa kwa siri kwa matumizi ya kijeshi katika kipindi cha kabla na wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia.
Viungo vya nje
haririMakala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
🔥 Top keywords: Maalum:TafutaMwanzoLuhaga Joelson MpinaUfahamu wa uwezo wa kushika mimbaOrodha ya mikoa ya Tanzania kwa eneoMikoa ya TanzaniaEe Mungu Nguvu YetuClatous ChamaTanzaniaNembo ya TanzaniaOrodha ya makabila ya TanzaniaKumaShairiMaalum:MabadalikoyaKaribuniIdara ya Usalama wa Taifa (Tanzania)VichekeshoDiamond PlatnumzFasihi simuliziOrodha ya Mawaziri Wakuu wa TanzaniaMaumivu ya kiunoMawasilianoKamusi za KiswahiliOrodha ya Makamu wa Rais TanzaniaMisemoOrodha ya nchi za AfrikaMfumo wa mmeng'enyo wa chakulaTendo la ndoaOrodha ya Watakatifu WakristoAina za manenoYoung Africans S.C.VitendawiliVita Kuu ya Pili ya DuniaMofimuShinikizo la juu la damuJumuiya ya Afrika MasharikiWasukumaJohn MagufuliKiswahiliMboo