The O.C. ni kipindi cha Marekani kilichohusu maisha ya vijana iliyoonyeshwa kuanzia 5 Agosti 2003 hadi 22 Februari 2007 kwenye Stesheni ya Fox Broadcasting Company. Kipindi hiki, kilichobuniwa na Josh Schwartz, kinahusu maisha ya kundi la vijana na familia zao wanapoishi mtaani Newport Beach kwenye mji wa Orange County, California.

The O.C.

Nembo ya The O.C.
AinaMaigizo ya vijana
Imetungwa naJosh Schwartz
ImeongozwaDave Bartis (season 1)
Bob DeLaurentis
Doug Liman (season 1)
McG
Stephanie Savage (season 4; co-executive producer seasons 1–3)
Josh Schwartz
Nchi inayotokaMarekani
LughaKiingereza
Ina misimu4
Ina sehemuOrange County, California
Utayarishaji
SehemuOrange County, California
Mudamakisio ni dk. 42
Urushaji wa matangazo
KituoFox
Inarushwa na5 Agosti 2003

The O.C. imeonyeshwa kwenye zaidi ya nchi 50 kote duniani na ilikuwa mojawapo ya vipindi maarufu mnamo 2003.[1] The O.C. ilivutia watazamaji milioni 9.7 katika msimu wake wa kwanza, lakini watazamaji walianza kupungua katika misimu iliyofuatia.

Stesheni zilizoonyesha kipindi hiki

hariri

Msimu wa kwanza ulianza saa tatu jioni mnamo 5 Agosti 2003 kwenye stesheni ya Fox nchini Marekani. Pia, ilionyeshwa nchini Canada kwenye stesheni ya CTV.[2][3]

Nchini Uingereza, kipindi cha kwanza kilianza mnamo 7 Machi 2004 saa tatu usiku kwenye stesheni ya Channel 4.[4]

Nchini New Zealand, kipindi hiki kilionyeshwa kwenye stesheni ya TG4.[5]

Nchini Afrika Kusini, ilianza 1 Aprili 2004 kwenye stesheni ya Go.[6]

Wahusika Wakuu

hariri
  • Peter Gallagher aliigiza kama Sandy Cohen, ambaye ni wakili, babake Seth na mumewe Kristen Cohen. Yeye anafungua ofisi yake ya kibinafsi na ni meneja. Mwishowe wa kipindi hiki, anakuwa profesa kwenye chuo cha Berkeley.
  • Kelly Rowan aliigiza kama Kristen Cohen. Yeye ni mkewe Sandy, na mamake Seth. Kabla ya kukutana na Sandy, yeye alipendana na Jimmy Cooper. Amewahi kupata shida ya kulewa.Baadaye, anakuwa mjamzito na mtoto huyo anaitwa Sophie Rose Cohen.
  • Benjamin McKenzie aliigiza kama Ryan Atwood, ambaye ni kijana matata. Mamake alimfukuza nyumbani, na baadaye anachukuliwa na Sandy Cohen kulelewa. Ryan anapendana na Marissa, lakini uhiusiano wao ulipata pandashuka tele. Mwishowe, Ryan na Marissa wanapata ajali barabarani na Marissa anakufa mikononi mwake.
  • Mischa Barton aliigiza kama Marissa Cooper, mpenzi wa Ryan. Yeye ni rafiki wa dhati wa Summer. Yeye pia amepata pandashuka nyingi, kama matumizi yamadawa ya kulevya.
  • Adam Brody aliigiza kama Seth Cohen. Yeye ni mpenzi wa Summer. Baadaye, anamuoa Summer.
  • Rachel Bilson aliigiza kama Summer Roberts, mpenzi wa Seth. Yeye ni mwana wa Dkt. Neil Roberts.

Mafanikio

hariri
MsimuVipindiSaaMwanzo wa msimuMwisho wa msimuMwakaNambaWatazamaji
(milioni)
127Jumanne saa 9:00 jioni (2003)
Jumatano saa 9:00 jioni (2003–04)
5 Agosti 20035 Mei 20042003–04#579.7[7]
224Alhamisi 8:00 p.m.4 Novemba 200419 Mei 20052004–05#857.0[8]
325Alhamisi saa 8:00 jioni (2005)
Alhamisi saa 9:00 jioni (2006)
8 Septemba 200518 Mei 20062005–06#1055.6[9]
416Alhamisi saa 9:00 jioni2 Novemba 200622 Februari 20072006–07#1234.3[10]

Logie Awards

hariri
  • Mnamo 2005, The O.C ilisinda tuzo la Most Popular Overseas Program.

PRISM Awards

hariri
  • Mnamo 2006, muigizaji Kelly Rowan alishinda tuzo la Performance in a TV Drama Series Episode.

Teen Choice Award

hariri
  • Mnamo 2004, Mischa Barton alishinda tuzo la Choice Breakout TV Star - Female.
  • Mwaka huo huo, Adam Brody pia alishinda tuzo la Choice TV Actor - Drama/Action Adventure.
  • Mwaka wa 2005, Rachel Bilson alishinda tuzo la Choice TV Actress:Drama.[11]

Marejeo

hariri
  1. Associated Press. "Fox's once hot 'The O.C.' canceled", Regina Leader-Post, 5 Januari 2007. Retrieved on 10 Februari 2007. Archived from the original on 2016-01-05. 
  2. McFarland, Melanie (5 Agosti 2003). "Fox's handsome 'The O.C.' may be just what teens crave". Seattle Post-Intelligencer. Hearst Corporation. Iliwekwa mnamo 24 Januari 2009.
  3. Gee, Dana. "Daring to do good: Role in the O.C. Peter Gallagher feels close to his", The Gazette, CanWest Interactive, 2 Agosti 2003. Retrieved on 9 Februari 2009. 
  4. Clark, Caren. "Switched on this week the best bits on TV", Southport Reporter, PCBT Photography, 6 Machi 2004. Retrieved on 16 Julai 2008. 
  5. Kenny, Colum (27 Agosti 2006). "Time to call a halt to the lip service behind TG4 'success'". Irish Independent. Iliwekwa mnamo 2009-09-14.
  6. "The O.C." TVSA. Iliwekwa mnamo 2009-09-14.
  7. "I. T. R. S. Ranking Report: 01 Thru 210". ABC Medianet. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-09-30. Iliwekwa mnamo 25 Mei 2007.
  8. "Primetime series". The Hollywood Reporter. Nielsen Business Media. 27 Mei 2005. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-05-19. Iliwekwa mnamo 12 Septemba 2009. {{cite web}}: Unknown parameter |= ignored (help); Unknown parameter |https://web.archive.org/web/20070519102605/http://www.hollywoodreporter.com/hr/search/article_display.jsp?vnu_content_id= ignored (help)
  9. "Series". The Hollywood Reporter. Nielsen Business Media. 26 Mei 2006. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2006-12-08. Iliwekwa mnamo 12 Septemba 2009. {{cite web}}: Unknown parameter |= ignored (help); Unknown parameter |https://web.archive.org/web/20061208201731/http://www.hollywoodreporter.com/hr/search/article_display.jsp?vnu_content_id= ignored (help)
  10. "2006–07 primetime wrap". The Hollywood Reporter. Nielsen Business Media. 25 Mei 2007. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-05-28. Iliwekwa mnamo 19 Juni 2009.
  11. "The Teen Choice Awards – Nominees", 20th Century Fox, 2005. Retrieved on 14 Agosti 2008. Archived from the original on 2008-02-05.