Vanadi ni elementi na metali ya mpito yenye namba atomia 23 na alama V katika mfumo radidia wa elementi. Ni metali laini na wayaikaji yenye rangi ya kifedha-nyeupe inayotokea katika madini na kampaundi mbalimbali.

Vanadi
Jina la ElementiVanadi
AlamaV
Namba atomia23
Mfululizo safuMetali
Uzani atomia 50.9415
Valensi2, 8, 11, 2
Densiti6.11 g/cm³
Ugumu (Mohs)6.7
Kiwango cha kuyeyuka2183 K (1910 °C)
Kiwango cha kuchemka3680 K (3407 °C)
Asilimia za ganda la dunia0.01 %
Hali maada mango

Inatumiwa kama sehemu za aloi za chumapua mbalimbali inapozuia kutu na kuongeza uwayaikaji wa chumapua. Aloi hizo zinatumiwa kwa vyombo vya kiganga kwa upasuaji, vipuri vya giaboksi, pamoja na titani katika aloi kwa matumizi ndani ya rafadha za injini za ndege.

Vanadi ina pia umuhimu fulani kwa miili ya viumbe ingawa wataalamu hawana uhakika bado vanadi inafanya kazi gani mwilini.

Picha

hariri