When You Tell Me That You Love Me

"When You Tell Me That You Love Me" ni wimbo uliotoka kama single mwaka 1991 kutoka kwa mwanamuziki wa nchini Marekani anayeitwa Diana Ross. Baadaye wimbo huu ulirudiwa kuimbwa na wanamuziki mbalimbali.

“When You Tell Me That You Love Me”
“When You Tell Me That You Love Me” cover
Single ya Diana Ross
MuundoCD, Vinyl (7" & 12")
AinaSoul
Urefu4:14
StudioMotown
MtayarishajiPeter Asher
Mwenendo wa single za Diana Ross
"No Matter What You Do"
(1991)
"When You Tell Me That You Love Me"
(1991)
"The Force Behind The Power"
(1991)

"When You Tell Me That You Love Me" ilikuwa ni single ilioongoza kutoka kwa albamu ya Diana Rose iliyotoka mwaka 1991, iliyoitwa The Force Behind the Power iliyotolewa na studio Motown nchini Marekani, na stdudio ya EMI ya nchini Uingereza.Wimbo huu wa mapenzi lakini yanayosikitisha ndio uliofanya vizuri zaidi katika albamu hii. Wimbo huu uliweza kufika nafasi ya 37# katika chati ya muziki ya Marekani ya Billboard na kushika nafasi ya 2# katika single 75 bora nchini Uingereza.Rose anauchukulia wimbo huu kama wimbo wenye kumatambulisha. [1] Toleo la nchini Uingereza lilijumuisha wimbo wake uliofanya vizuri mwaka anaoitwa "Chain Reaction." [2]

Muziki wa Video

hariri

Video ya muziki huu ilitoka ikiwaonesha Ross akiwa katika gauni la jioni, akiwa anaimba katika jukwaa, na kuingiza picha zingine zikimwonesha Ross akiwa na watoto wake wawili wa kiume, Ross & Evan. [3]

Orodha ya nyimbo

hariri

UK Vinyl, 12" (12 EM 217)[4]

  1. When You Tell Me That You Love Me (LP Version) (4:14)
  2. Chain Reaction (12" Version) (3:50)
  3. You And I (4:06)

UK CD Maxi (CDEM 217, 20 5600 2 )[5]

  1. When You Tell Me That You Love Me (LP Version) (4:14)
  2. Chain Reaction (12" Version) (3:50)
  3. You And I (4:06)

US Vinyl, 12" (L33-1643 )[6]

  1. When You Tell Me That You Love Me (LP Version) (4:10)
  2. When You Tell Me That You Love Me (LP Version) (4:10)

US Cassette Single" (MOTCS-2139 )[6]

  1. When You Tell Me That You Love Me (LP Version) (4:10)

Chati

hariri
Chati (1991)Ilipata
nafasi
UK Singles Chart2
Hot R&B/Hip-Hop Songs37

Toleo la Julio Iglesias

hariri
“When You Tell Me That You Love Me”
Single ya Julio Iglesias na Dolly Parton
Muundo5" CD Single
AinaPop, soul
Urefu3:59
StudioColumbia Records
MtunziAlbert Hammond na Bettis

Wimbo huu ulirekodiwa tena, kwa Dolly Parton kushirikiana na Julio Iglesias kwa ajili ya lalbamu yao ya mwaka 1994 iliyoitwa Crazy. Single hii ilitoka mwaka 1995 na kufanikiwa kuingia katika chati ya muziki ya Uholanzi na kukaa kwa kipindi cha takribani wiki tatu. Wimbo huu uliingia katika chati hii na kushika nafasi ya 48# na baadae nafasi ya 45# la mwishoni ilishika nafasi ya 49# [7]

Kwa mujibu wa Iglesias, Parton alikuwa mmoja kati ya wanamuziki aliopenda kufanya nao kazi. Parton alijumuisha wimbo huu katika diski yake ya The Tour Collection. [8]

Miziki wa Video

hariri

Video ya muziki ilifanyika katika Jumba la Oheka lililipo katika kisiwa cha Long Island kaskazini mwa ufukwe wa bahari. Katika toleo lingine, Iglesias na Parton wanaonekana kuimba katika vyumba tofauti tofauti, la hali ya mapenzi kuwatawala. Mwishoni mwa video anaonekana Parton na Iglesias wakiwa wanatoka katika jumba hilo, huku Parton akiwa amebadilisha kutoka gauni lenye rangi jeupe kwenda gauni jeusi[9]

Chati

hariri
Chati (1995)Ilipata
nafasi
Dutch Top 40[7]45

Toleo na CoCo Lee

hariri

Mwaka 1998 Iglesias alirudia kurekodi wimbo huo na mwanamuziki kutoka nchini China anayeitwa Coco Lee (李玟) ulitoka kama single katika kutangaza mkusanyiko wake wa nyimbo zilizoitwa My Life: The Greatest Hits. lakini pamoja na haya, toleo la Coco halikujumuishwa katika albamu yake na badala yake likajuimshwa lile la Parton. [10] Video ya Muziki ilitoka ikimwonesha Iglesias na Lee wakiwa katika studio ya kurekodia. mwishoni, Iglesias na Lee wanaonekana wakiwa wamekaa katika chakula cha jioni. [11]

Toleo la Westlife

hariri
“When You Tell Me That You Love Me”
Single ya Westlife and Diana Ross
kutoka katika albamu ya Face To Face
MuundoCD Single
AinaPop, soul
StudioSony BMG
CertificationSilver
"You Raise Me Up"
(1)
"When You Tell Me That You Love Me"
(2)
"Amazing"
(3)

Diana Ross alirekodi kwa mara ya pili wombo wake wa When You Tell Me That You Love Me na kundi kutoka nchini Ireland la Westlife, mwaka 2005 katika albamu yao inayoitwa Face To Face Ilikuwa ni single ya pili katika albamu hii.Wimbo huu ulishika nafasi ya thelathini na tisa katika nyimbo zilizoongoza kwa mauzo nchini Uingereza kwa mwaka 2005

Orodha ya nyimbo

hariri

CD ya kwanza

hariri
  1. When You Tell Me That You Love Me (With Diana Ross) (Single Mix)
  2. White Christmas
  3. The Way You Look Tonight (Westlife Only Version)

CD ya pili

hariri
  1. When You Tell Me That You Love Me (With Diana Ross) (Single Mix)
  2. If I Let You Go (Acoustic Version)

Chati

hariri
Chati (2005)Ulipata
nafasi
Dutch Top 40[12]45
Irish Singles Chart2
UK Singles Chart2

Viungo vya nje

hariri

Marejeo

hariri
🔥 Top keywords: