Wilaya ya Laikipia


Wilaya ya Laikipia ilikuwa moja kati ya wilaya sabini na moja za Jamhuri ya Kenya hadi ilipopitishwa katiba mpya ya nchi (2010).

Wilaya ya Laikipia
Mahali paWilaya ya Laikipia
Mahali paWilaya ya Laikipia
Mahali pa Wilaya ya Laikipia katika Kenya
NchiBendera ya Kenya Kenya
Mji mkuuNanyuki
Eneo
 - Jumla8,696.1 km²
Idadi ya wakazi (2009 Sensa[1])
 - Wakazi kwa ujumla 399,227

Ilikuwa wilaya mojawapo ya Mkoa wa Bonde la Ufa iliyoko kwenye Ikweta.

Makao makuu yalikuwa mjini Nanyuki.

Kwa sasa imekuwa kaunti ya Laikipia.

Wilaya hii ilikuwa na vituo viwili vikuu vya soko: Nanyuki kwenye upande wa kusini mashariki, na Nyahururu kwenye upande wa kusini magharibi.

Wakikuyu walikuwa takribani 60% ya idadi ya watu wote kwenye wilaya hii, huku idadi iliyosalia ikijumuisha watu wa makabila mengine, ni pamoja na Mukogodo Masai, Wasamburu, Wameru, Waborana, Wakalenjin, Wasomali, Wazungu, Watu wa asili ya Asia, na Waturkana, wakiipa wilaya hii idadi ya watu tofauti tofauti. Mashamba mengi yanamilikiwa na idadi ndogo ya masetla wa ukoloni.

Shughuli kuu za kiuchumi katika wilaya hii ni utalii na kilimo, haswa mimea za mbegu, ufugaji na kilimo cha maua,matunda na mboga.

Hali ya hewa ya wilaya hii ni ya baridi kiasi, ikiwa na msimu wa mvua na kiangazi.

Serikali za Mtaa (Mabaraza)
BarazaAinaIdadi ya Watu*Wakaazi wa mjini*
NanyukiManispaa39,83831,577
NyahururuManispaa32,12024,751
RumurutiMji31,6494,249
LaikipiaKaunti218,5803,610
Jumla-322,18764,187
* 1999 census. Source: [1]
Maeneo ya utawala
TarafaIdadi ya Watu*Wakaazi wa mjini*Makao makuu
Mkoa wa Kati77,47828,489Nanyuki
Lamuria38,5170Lamuria
Mukogondo13,176624
Ngarua65,5452,813Kinamba
Nyahururu37,41222,459Nyahururu
Olmoran11,0690
Rumuruti78,8944,061Rumuruti
Jumla322,18758,466-
* 1999 census. Sources: [2], [3],

Wilaya hii ina Majimbo ya Uchaguzi mawili:

Marejeo

hariri

Viungo vya nje

hariri